October 9, 2017

BANDA 

Beki kiraka anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Abdi Banda, ameweka bayana kuwa kutokana na uimara wa kikosi cha Simba cha sasa uliochagizwa na usajili kabambe wa nyota kama Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima kwenye kikosi hicho, ana uhakika mkubwa wa nyota hao kuibeba timu hiyo na kutwaa ubingwa msimu huu.

Banda ambaye alikuwa sehemu ya Simba kwa msimu uliopita ambayo iliukosa ubingwa wa ligi dakika za mwisho, ameondoka msimu huu na kutimkia Afrika Kusini ndani ya Klabu ya Baroka ambayo amejiunga nayo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Banda amesema kuwa ana imani kubwa juu ya wachezaji waliopo sasa wanaweza kulibeba jahazi la timu hiyo kutokana na uzoefu wao mkubwa kwenye mashindano mbalimbali pamoja na uchu wao wa mataji jambo ambalo linampa uhakika kabisa Simba lazima itwae ubingwa msimu huu.

“Mimi binafsi nina imani kubwa sana na kikosi hiki cha sasa cha Simba kwamba msimu huu lazima kifanye jambo kubwa na kufuata nyayo zetu ambazo tuliziacha kwa msimu uliopita baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho (FA), wao wana uwezo kabisa wa kuchukua ubingwa wa ligi.

“Nasema hivyo kwa sababu ya kufanyiwa kwa marekebisho makubwa kwenye timu hasa kwa kuwaleta nyota wenye viwango vya juu kama Okwi na wengineo ambao wanajua nini wafanye ili watwae ubingwa, kwa upande wangu naona kabisa msimu huu ile kiu ya ligi itakatwa,” alisema Banda.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic