October 7, 2017



Taifa Stars leo Jumamosi inacheza mechi ya kirafiki na Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Sh 3,000 na kikubwa ni Sh 5,000.

Kuelekea mchezo huo, nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, amesema wana uhakika wa kushinda leo kutokana na maandalizi waliyofanya kambini.

Mchezo huo ambao upo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), unatolewa macho na timu zote mbili kama sehemu ya kujiandaa na mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa Afrika 2019.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Malawi, Ronny van Geneugden, amesema: “Tanzania tunaifahamu ni timu nzuri na inatoa ushindani ukikutana nayo, tulikutana nayo katika Cosafa Cup naamini ni kipimo
kizuri kwetu.”

Naye Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amesema: “Vijana wangu wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo), kikosi hiki kitanipa taswira ya timu
yetu ambayo inaelekea kucheza mechi za kufuzu Afcon 2019.”

Nahodha Samatta aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao huku akisema mchezo huo una umuhimu kwao kujitengenezea nafasi ya kupanda kwenye viwango vya Fifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic