October 19, 2017


Siku moja baada ya kuamua kuondoka Simba, imeelezwa kuwa Kocha Jackson Mayanga ana mpango wa kujiunga na Kagera Sugar.

Taarofa zinaeleza, Mayanja anakwenda Kagera Sugar kuchukua nafasi ya Mecky Maxime ambaye mambo yamemuendea vijana.

Jana jioni, kiongozi mmoja wa Kagera Sugar aliyedai si msemaji wa klabu, alisema wanamhitaji Mayanja lakini hawahusiki na kuondoka kwake Simba.

“Tuliwahi kuzungumza na Mayanja tuliposikia Simba wanataka kumuacha. Lakini kwa sasa naweza kusema bado tunamtaka akiwa na nafasi.

“Lakini hatujashinikiza aondoke Simba na kama ikitokea yuko free, tunaweza kuzungumza naye kuangalia namna ya kuongeza nguvu,” alisema.

Hata hivyo, kiongozi huyo alikataa katakata kuzungumzia suala la Maxime kama anaondoka au anaendelea kubaki.


“Hilo la Maxime tuliache kwa sasa,” alisema kwa ufupi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic