October 14, 2017




Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema kama wangekuwa wanakutana na Yanga ndani ya wiki hii, basi mchezaji wa kuchungwa zaidi ni Ibrahim Ajibu Migomba.

Hans Poppe amesema safu ya ushambulizi ya Yanga si ya kutisha sana katika kipindi hiki labda kama kutakuwa na mabadiliko baadaye.

Katika mahojiano na SALEHJEMBE, Hans Poppe amesema, angalau Ajibu anaonyesha kuwa yuko vizuri kutokana na kuonyesha anapambana pamoja na kufunga.

“Sidhani kama wanatisha labda wabadilike. Lakini kama utazungumzia mchezaji hatari basi ni huyu aliyetoka kwetu, Ajibu.

“Hawa wengine Ngoma (Donald), Tambwe (Amissi) na Chirwa (Obrey) naona
si wale ambao tuliwazoea. Sijui sababu ya majeruhi au vipi,” alisema.

Hata hivyo, Hans Poppe alikataa kuizungumzia kwa undani mechi dhidi ya Yanga ambayo itapigwa Oktoba 28, mwaka huu akisema wanaangalia mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kesho na ile watakayoivaa Njombe Mji.

Ajibu amejiunga na Yanga akitokea Simba baada ya kuona hakuwa amepata alichokuwa anahitaji.

Kwa kipindi hiki, Ajibu ambaye amekulia kisoka katika Klabu ya Simba, ndiye tegemeo zaidi katika kikosi cha Yanga hasa katika safu ya ushambulizi.


Yanga imefunga mabao manne tu ya ligi kuu huku Ajibu akiwa amefunga mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic