October 14, 2017

KIUNGO SAID NDEMLA AKIJARIBU KUMZUIA HARUNA NIYONZIMA KWA KUMVUTA JEZI BAADA RAIA HUYO WA RWANDA KUMTOKA KATIKA MAZOEZI YA SIMBA JIJINI DAR, LEO.

Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, leo ameonyesha anaanza kupanda katika kiwango anachokitaka.

Niyonzima ambaye hivi karibuni alianza mazoezi ya ziada kuhakikisha anakuwa katika kiwango chake, leo amekuwa kivutio katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Niyonzima alionyesha kiwango kizuri wakati walipogawanywa kuchezwa kama timu na kufanya baadhi ya mashabiki waliokuwa pale kuanza kumjadili.

“Inaonekana kiwango kinaanza kurejea, mazoezi ya ziada yanaweza kuwa yameanza kulipa,” alisema shabiki mmoja na kuwachekesha wenzake.


Niyonzima alisema kiwango chake hakipo anavyotaka na kueleza sababu ya kutopata maandalizi ya kutosha mwanzoni mwa msimu wakati akijiunga na Simba akitokea Yanga.

Tayari amekuwa akifanya mazoezi ya ziada ufukweni pia katika gym kuhakikisha anajiimarisha zaidi.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic