October 18, 2017


Kocha Jackson Mayanja ameamua kuachana na klabu ya Simba na krejea kwao Uganda.

Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo yake binafsi.

“Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema.


Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake baada ya kukubaliana naye kutokana na uamuzi wake huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic