Mtoto wa kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima ameamua kuvaa jezi za Simba kumsapoti baba yake.
Niyonzima amesema mwanaye huyo amemuomba baba yake kumnunulia jezi za Simba jambo ambalo amelifanya.
“Alianza kuniambia baba mimi nataka kuvaa jezi za Simba, jambo ambalo mimi siwezi kulipinga kwa kuwa ni chaguo lake,” alisema Niyonzima wakati akihojiwa na kipindi cha SPOTI HAUSI cha Global Tv Online.
“Kabla ya hapo alipenda kuvaa jezi za Yanga wakati mimi nikiwa Yanga, aliposikia nimejiunga na Simba, moja kwa moja akataka nimnunulie jezi za Simba jambo ambalo nililifanya mara moja.”
Niyonzima alionyesha kiwango cha juu wakati Simba ikiivaa Mtibwa Sugar katika mechi iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 Simba wakisawazisha mwishoni kabisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment