October 3, 2017



Nahodha wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amesema wanataka kuendelea kushinda baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Yanga.

Nditi amesema wamefanikiwa kupata sare na Yanga katika mechi ambayo anaamini kipindi cha kwanza walitakiwa kushinda lakini mechi zijazo lazima waendeleze mwendo mzuri wa ushindi waliokuwa nao.

“Unajua mechi na Yanga ilikuwa ngumu mwishoni, lakini kipindi cha kwanza tulifanya vizuri zaidi. 

“Baada ya mechi hiyo tunaangalia mbele, tunataka kushinda, tunataka kufanya vizuri zaidi na kuendelea hivyo hadi mwisho wa ligi.

“Kila mmoja anajua ligi ni ngumu lakini uchezaji wa nidhamu na malengo, utatufanya tuendelee kufanya vizuri,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic