October 12, 2017



Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma ataifuata timu yake mjini Shinyanga.

Yanga inaondoka leo kwenda mjini Bukoba ikipitia Mwanza kwenda kuivaa Kagera Sugar.

Ngoma na Thabani Kamusoko wanaachwa Dar es Salaam ili kuendelea na matibabu kutokana na kuwa majeruhi.

Lakini Ngoma, atakwenda Shinyanga kwa kuwa atakuwa amerejea katika hali yake.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema baada ya mechi ya Jagera, watakwenda Shinyanga kuivaa Stand United ambako Ngoma ataungana nao.

"Wakati tukiwa Shinyanga tutaungana na Ngoma. Daktari amesema atakuwa amerejea katika hali nzuri," alisema.

Yanga inapaa na "pipa" kwenda mjini Mwanza baadaye Bukoba kwa ajili ya mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, wikiendi hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic