October 25, 2017




Klabu ya Yanga imeanza kukisuka kikosi chake cha wanawake kitakachoshiriki Ligi Kuu Bara.


Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa ndiye atafanya kazi ya kuchagua wachezaji sahihi.

Makamu Mwenyekiti wa timu ya wanawake, Siza Lyimo amesema Mkwasa kwa kuwa ni kocha na mtaalamu katika soka la wanawake.

"Mkwasa ndiye atakayefanya kazi hiyo kupata watu ambao ni sahihi kwa ajili ya kikosi chetu," alisema.

"Baada ya hapo litafuatia suala la usajili na Mkwasa atalisimami. Zoezi litaanza Oktoba 25, tunawakaribisha wote wenye vipaji."

Katika hatua nyingine timu hiyo leo Jumanne imetambulisha timu yao ya wanawake, Yanga Princess ambayo itashiriki Ligi Kuu ya Wanawake Bara ambayo itaanza hivi karibuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic