October 25, 2017



Kikosi cha Yanga leo Jumanne kimetua mkoani Morogoro ambapo kitaweka kambi yake ya muda mfupi kabla ya kuwavaa wapinzani wao, Simba Jumamosi hii kwa wachezaji wote kuwemo kwenye kambi hiyo chini ya Mzambia, George Lwandamina.

Katika hatua nyingine Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuzingatia idadi ya mashabiki ambao watatosha ndania ya uwanja huo, ambapo wao wamepewa nafasi za mashabiki elfu kumi na moja pekee (11,000).

“Hatutaki yatokee maafa uwanjani, tunataka idadi ya mashabiki wakijaa uwanjani basi wengine wasije waangalie namna nyingine ya kuangalia mechi hii, uwanja unakusanya mashabiki 22,000 tu tunataka pakijaa basi wasiongezeke,”alisema Mkwasa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic