November 28, 2017


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwa mara nyingine amewazungumzia mashaa wake wawili, Alexis Sanchez na Mesut Ozil kwa kusema kuwa wataendelea kuichezea timu hiyo hadi mwisho wa msimu na kusisitiza kuwa hana mpango wa kuwauza Januari, mwakani.

Kumekuwa na taarifa kuwa wachezaji hao wanaweza kuondoka kwa kuwa mikataba yao inaelekea ukingoni na hawajafikia makubaliano ya kusaini mikataba mipya, ili kuokoa fedha, ilielezwa kuwa Arsenal ingewauza karika usajili wa dirisha dogo la Januari, mwakani. 

“Kichwani mwangu wataendelea kubaki hapa hadi mwisho wa msimu, labda kama kuna kitu cha ajabu kitatokea.

“Kumekuwa na taarifa nyingi, je wataendelea kubaki hapa kwa muda mrefu? Hilo ni swali gumu kulijibu kwa sasa,” alisema Wenger.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic