November 18, 2017


Kwa mambo yalivyo, huenda kesho Jumapili ikamtumia beki wake wa kushoto Haji Mwinyi katika mchezo dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam badala ya Gadiel Michael.

Katika mechi tisa za ligi kuu msimu huu, zote Gadiel ameanza huku Mwinyi akiwa katika benchi lakini kwa mujibu wa mazoezi ya jana, Mwinyi leo anaweza kucheza.

Mazoezini ya jana Mwinyi alianza katika kikosi ambacho kilionekana kuwa cha kwanza katika mchezo wa leo huku Kocha George Lwandamina akionekana kuwa makini naye.

Mwinyi alionyesha uwezo mzuri katika mazoezi hayo huku akimzuia vilivyo winga Geoffrey Mwashiuya ambaye hupata nafasi kikosi cha kwanza katika siku za hivi karibuni.

Pia Lwandamina alionekana akiwajaribu Pato Ngonyani na Raphael Daudi katika nafasi ya kiungo mkabaji kwani Papy Kabamba Tshishimbi, hatakuwepo kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.

Katika mazoezi hayo, ilionekana Raphael ndiye atakayeanza huku katika beki ya kati nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ naye akionekana kurudi kikosi cha kwanza kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani ambaye hakufanya mazoezi jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic