Kuna zile taarifa kuwa Simba na Yanga zote zinamuwania straika wa Prisons, Mohammed Rashid lakini klabu yake hiyo imezionya timu hizo na kusema mchezaji huyo ataziponza.
Simba na Yanga zinamtaka Rashid mwenye miaka 22 na ambaye amekuwa akifanya vizuri katika ligi akiwa na mabao sita ambayo ni mawili nyuma ya Emmanuel Okwi anayeongoza kwa ufungaji ligi kuu.
Katibu Mkuu wa Prisons, Havinitishi Abdallah amesema hawatakuwa tayari kumuachia Rashid aondoke pia kanuni
haziruhusu kwa timu yoyote kuzungumza naye.
“Tuna mkataba na Rashid wa miaka miwili, sasa inakuwaje timu zinazungumza naye? Huyu anaziponza timu zinazozungumza naye kwani ni kinyume na kanuni.
“Mchezaji aliyebakisha mkataba wa miezi sita ndiye anaweza kuzungumza na timu nyingine kuhusu usajili mpya lakini siyo huyu wetu mwenye
miaka miwili.
“Hatupo tayari kumuacha Rashid aondoke, na hata hizo timu zinazomtaka zikiendelea na mazungumzo naye tukipata ushahidi tutazishitaki,” alisema Abdallah.








0 COMMENTS:
Post a Comment