November 26, 2017

Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Twiga Stars, Edna Lema akiteta na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Uwanja wa General Tyre, katika  mchezo wa ufunguzi Alliance Queens wameshinda 2-1 dhidi ya Panama FC.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi  katika mchezo wa uzinduzi wa Ligi Kuu Soka ya Wanawake, imefahamika.


Kundi A lina timu za Mlandizi Queens ya Pwani, JKT Queens ya Dar es Salaam, Fair Play ya Tanga, Simba Queens ya Dar es Salaam, Ever Green Queens ya Dar es Salaam na Mburahati Queens ya Dar Es Salaam.

Kundi B lenyewe linajumuisha timu za Marsh FC ya Mwanza, Kigoma Sisters ya Kigoma, Panama FC ya Iringa, Baobab Queens ya Dodoma, Alliance Queens ya Mwanza na Majengo Queens ya Singida.

Katika mchezo wa ufunguzi mkoani Arusha katika Kundi B, Panama FC imepoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Alliance Queens, bao la Panama likifungwa na Neema wakati yale ya washindi yakiwekwa wavuni ni Mwamvita na Ester.

Katika kituo cha Dar kwenye Uwanja wa Karume JKT Queens imegawa dozi nzito ya mabao 9-0 dhidi ya Mlandizi Queens.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic