November 12, 2017



Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina anarejea nchini kesho tayari kujiunga na kikosi chake.

Lwandamina alikuwa kwao nchini Zambia ambako alikwenda kuhani msiba wa mdogo wake.

“Kocha hakuwa amepata nafasi ya kwenda msibani, sasa aliona akitumie kipindi hiki kwenda msibani kabla ya kurejea haraka,” kilieleza chanzo.

Lwandamina ataunga na kikosi chake katika mazoezi ya keshokutwa wakati kitakapokuwa kinarejea katika mazoezi ya uwanjani.


Kesho, Yanga wataanza mazoezi ya gym kabla ya kuanza mazoezi ya uwanjani keshokutwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic