November 24, 2017





Straika wa Yanga, Matheo Antony amelazimika kunyoa rasta ili kuweza kuungana na timu yake ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ambayo inatarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji.

Matheo ni mmoja wa washambuliaji walioitwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Hemed Morocco kushiriki michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

“Imenibidi ninyoe rasta zangu kwa sababu katika kikosi cha Zanzibar Heroes haturuhusiwi kuwa na mitindo yoyote ile, ndiyo imenibidi nifanye hivyo.


“Ni jambo la busara kusikiliza kile ambacho mwalimu anakuelekeza na kufuata, kwa hiyo mimi nimeridhia ndiyo maana niko hivi kama unavyoniona na hakuna tatizo,” alisema Matheo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic