Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Novemba 22, 2017 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi kwa msimu wa 2017/2018 inayoendelea hivi sasa.
JKT Mlale imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya KMC kumchezesha nahodha wake Stephano Mwasyika katika mechi namba 28 iliyofanyika Oktoba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex wakati akiwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Mwasyika alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko mpinzani wake kwenye mechi namba 15 kati ya KMC na Mbeya kwanza iliyochezwa Oktoba 5, 2017 katika Uwanja wa Azam Complex.
Baada ya kupata kadi hiyo, Mwasyika alitakiwa kukosa mechi tatu na kulipa faini ya sh. 300,000 (laki tatu). Mechi alizotakiwa kukosa ni dhidi ya Mufindi United (Oktoba 15), Polisi Tanzania (Oktoba 23) na JKT Mlale (Oktoba 30). Alikosa mechi mbili tu za kwanza, lakini akacheza mechi ya tatu dhidi ya JKT Mlale iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment