November 23, 2017







Kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, Bodi ya Ligi Tanzania Bara imekaa kikao na kufikia maamuzi mbalimbali katika Ligi Daraja la Kwanza.


Klabu ya Toto Africans imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kikao cha maandalizi (pre match meeting) katika mechi dhidi ya Biashara United Mara iliyofanyika Novemba 5, 2017 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Adhabu hiyo ni utekelezaji wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Meneja wa Toto Africans, Yusufu Jumaa amefungiwa miezi miwili na kupigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) baada ya kuondolewa na Mwamuzi kwenye benchi la ufundi kwa kupinga maamuzi yake na kumshambulia kwa maneno.

Ofisa Habari wa Toto Africans, Cuthbert Japhet amesimamishwa hadi suala lake la kummwagia maji Mwamuzi na kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali wakati wa mapumziko katika mechi hiyo litakaposilikizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Waamuzi Wasaidizi Jumanne Njige wa Mwanza na Bam Bilasho wa Dodoma wamepewa Onyo Kali kwa kuchezesha chini ya kiwango mechi namba 36 ya Kundi C kati ya Transit Camp na Rhino Rangers iliyofanyika Novemba 11, 2017 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 38(5) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic