November 15, 2017


Kiungo wa Simba, Said Hamis Ndemla anaendelea na majaribio katika klabu ya AFC ya Sweden.

Ndemla anaendelea kufanya majaribio hayo tokea juzi Jumatatu na leo itakuwa ni siku yake ya tatu akifanya majaribio hayo.

Kikosi cha AFC kinachojiandaa na mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu Sweden, kinamjumuisha Ndemla ambaye ameungana na wachezaji wa kikosi hicho katika mazoezi.


Ndemla amepewa siku 14 za majaribio kumuonyesha kocha na benchi la ufundi alichonacho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic