November 14, 2017

PICHA KWA HISANI YA SAMATTA;
Unaweza kushangaa lakini ndiyo mambo ya Ulaya kwani Mtanzania, Mbwana Samatta ameanza mazoezi mdogomdogo.

Samatta anaonekana akiwa ameanza mazoezi ya gym siku chache tu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.


Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars aliumia wakati akiichezea timu yake ya Genk dhidi ya Lokeren katika Ligi Kuu ya Ubelgiji, wiki iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV