November 13, 2017



Huku kukiwa na taarifa kwamba wachezaji wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe wanaweza kuhamia Singida United, Kocha wa kikosi hicho Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amemaliza mjadala huo.

Pluijm amesema hana mpango kabisa na wachezaji hao na anajua wana mkataba na klabu yao ya Yanga.

Tetesi zimeenea kuwa huenda wachezaji hao wakatemwa ndani ya kikosi hicho kutokana na kuandamwa na majeraha.

Pluijm alisema kuwa sasa ameelekeza nguvu zake katika kufanyia kazi upungufu kwenye kikosi chake na siyo kufikiria kumsajili Tambwe na Ngoma. 
“Hizo taarifa za kusema nataka kuwasajili Ngoma na Tambwe si kweli kwa sababu nafahamu wale wachezaji wapo kwenye mikataba na klabu yao hilo naliheshimu na sitaki kuliingilia.


“Zaidi napambana kuhakikisha naendelea kuijenga timu yangu kwa bidii hasa katika upande wa safu ya ushambuliaji ndiyo ninaifanyia kazi kwa kiasi kikubwa, masuala ya usajili kwa sasa siwezi kuyazungumzia,” alisema Pluijm.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic