November 2, 2017



Yule Mnigeria, Mussalawal Ibrahim aliyepewa nafasi ya kufanya majaribio na kufulia, imeelezwa hakuwa na uwezo badala yake ulikuwa mchongo wa mwanachama mmoja ambaye aliwapelekea viongozi.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema mwanachama huyo alimpeleka Ibrahim kwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji akimshawishi kuwa jamaa ni hatari.

"Baada ya kiongozi kushawishiwa, yeye akasema apewe nafasi ya majaribio. Basi yule mwanachana akawa kila siku anapiga simu kushawishi kuwa ana uwezo.

"Alifika siku ambayo kocha Masoud Djuma alijiunga na Simba. Lakini tokea siku hiyo hakuna alichoonyesha ndiyo maana viongozi walipoenda Zanzibar wakasisitiza aondoke," kilieleza chanzo.


1 COMMENTS:

  1. Ndo maana simba watateseka sana kuupata ubingwa. Sajili zao nyingi ni kwa matakwa ya wanachama wao na si Kocha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic