December 8, 2017





Kiungo makabaji wa Yanga raia wa DR Congo Pap Tshishimbi Kabamba, kwa mara nyingine leo ameamsha molari ya wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuanza moja kwa moja mazoezi ya pamoja na wenzake yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Tshishimbi ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu wake aliyoyapata kwenye moja ya mazoezi yao  siku chache kabla ya Ligi Kuu Bara, kusimama kupisha michezo ya kimataifa.


Kiungo huyo ambaye alianza mazoezi ya gym, leo alionekana yuko fiti na ataendelea kujiboresha kadiri muda unavyosonga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic