December 11, 2017

Kiungo matata wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Ibrahim Ajibu amefunguka kuwa hawakuwa na bahati tu katika michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya, kwani walipambana.

Ajibu ameyasema hayo ikiwa ni siku chache tu baada ya Kilimanjaro Stars kupoteza mchezo wake dhidi ya Rwanda kwa mabao 2-1, kwenye muendelezo wa michuano hiyo juzi Jumamosi nchini Kenya. Kwa sasa Kilimanjaro Stars wanaofundishwa na kocha Ammy Ninje hawana matumaini ya kusonga mbele baada ya kupata pointi moja kwenye michezo mitatu.

Ajibu anayeitumikia Yanga amesema kuwa licha ya matokeo kuwaendea kinyume na matarajio yao, wao walipambana inavyotakiwa. 

“Kiukweli kama wachezaji tulikuwa tunapambana sana uwanjani kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri ya kikosi chetu lakini ndiyo hivyo mwisho wa siku mambo yanakuwa tofauti na vile ambavyo tulikuwa tunatarajia, tangu mchezo wa kwanza umeanza tulikuwa tunataka tushinde lakini ikawa tofauti.

“Kwa sasa tunaenda kujiandaa na michuano mingine itakayokuja kwani hii mambo hayajaenda kama ambavyo tulipanga baada ya kufika huku, tutajitahidi tufanye vizuri kwenye mchezo unaokuja,” alisema Ajibu.  

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Ibrahim Ajibu amefunguka kuwa hawakuwa na bahati tu katika michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya, kwani walipambana.

Ajibu ameyasema hayo ikiwa ni siku chache tu baada ya Kilimanjaro Stars kupoteza mchezo wake dhidi ya Rwanda kwa mabao 2-1, kwenye muendelezo wa michuano hiyo juzi Jumamosi nchini Kenya. Kwa sasa Kilimanjaro Stars wanaofundishwa na kocha Ammy Ninje hawana matumaini ya kusonga mbele baada ya kupata pointi moja kwenye michezo mitatu.

Ajibu anayeitumikia Yanga amesema kuwa licha ya matokeo kuwaendea kinyume na matarajio yao, wao walipambana inavyotakiwa. 

“Kiukweli kama wachezaji tulikuwa tunapambana sana uwanjani kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri ya kikosi chetu lakini ndiyo hivyo mwisho wa siku mambo yanakuwa tofauti na vile ambavyo tulikuwa tunatarajia, tangu mchezo wa kwanza umeanza tulikuwa tunataka tushinde lakini ikawa tofauti.

“Kwa sasa tunaenda kujiandaa na michuano mingine itakayokuja kwani hii mambo hayajaenda kama ambavyo tulipanga baada ya kufika huku, tutajitahidi tufanye vizuri kwenye mchezo unaokuja,” alisema Ajibu.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic