MNYATE |
Kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola amewaambia Simba wampe Juma Liuzio na Jamal Mnyate kutokana na wao kutowatumia huku yeye akiwa na mahitaji nao kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake.
Liuzio na Mnyate hivi sasa wamekuwa hawana nafasi katika kikosi cha Simba na mara kadhaa wamekuwa wakiishia benchi kutokana na kikosi hicho kuwa na nyota wengi.
Akizungumza na katika kipindi cha Spoti Hausi kinachorushwa na Global TV Online kila Alhamisi kuanzia saa 10:00 jioni, Matola alisema kuwa kama Simba hawawataki wachezaji hao, basi wampe yeye hata kwa kumuuzia ili aongeze nguvu katika kikosi chake,” alisema Matola.
Kutazama mahojiano hayo kamili tembelea chaneli ya Global TV Online kwenye YouTube.
0 COMMENTS:
Post a Comment