Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI maarufu ya kuuza matairi nchini ya Bin Slum Tyres Ltd, inajulikana sana nchini kutokana na sifa ya ubora wa bidhaa zake.
Ubora wa bidhaa zake kama Double Stars, Vee Rubber, Topu Steel Wheel na RB Battery zimekuwa zikiipaisha kampuni hiyo na kufanya watu wengi kuona kama kila matairi yanayopatikana nchini, husambazwa au kuuzwa na Bin Slum Tyres.
Umaarufu huo ni wa ubora lakini hali ya uamuzi wa kampuni hiyo kurudisha kwa jamii kupitia michezo, imefanya umaarufu wake kupanda kwa kiasi kikubwa.
MKURUGENZI MTENDAJI MKUU WA BIN SLUM TYRES LTD, NASSOR BIN SLUM |
Makampuni mengi ambayo ni makubwa huenda hata Bin Slum Tyres Ltd, yamekuwa magumu kuwekeza katika jamii au kujitoa katika michezo ambayo ni sehemu ya jamii.
Uoga wao unatokana na mambo mengi, wako hawajui umuhimu wa jamii lakini wengine wamekuwa waoga kuwekeza katika michezo kutokana na uoga wa mambo kwenda mlama.
Kwamba wanaweza wakaingiza fedha zao lakini mwisho kukawa na migogoro na mwisho wasione faida ya wao kudhamini katika michezo.
Kawaida, mfanyabiashara angependa kuwekeza naye apate matokeo ambayo yatamsaidia katika biashara yake.
Lakini Kampuni ya Bin Slum Tyres imeonyesha mapenzi makubwa katika michezo bila ya kujali yote hayo na imeyashangaza na kuyashawishi makampuni mengi kuingia katika kudhamini michezo hasa soka.
Misimu kadhaa ya Ligi Kuu Bara iliyopita, Bin Slum Tyres ilidhamini timu tatu kwa wakati mmoja ambazo ni Mbeya City, Ndanda FC na Stand United na hiyo ilikuwa rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na kampuni yoyote hadi SportPesa walipoifikia msimu huu baada ya kuzidhamini Simba, Yanga na Singida United.
Ingawa wameifikia bado unaona kuna tofauti kwa Bin Slum Tyres kuzidhamini hata timu zisizokuwa na majina tena zinazotokea mikoani badala ya zile kubwa na maarufu sana kama ilivyozoeleka.
Ukiangalia Ndanda na Stand baadaye wote walipata wadhamini ambao waliona inawezekana baada ya Bin Slum Tyres kuwadhamini ambalo ni jambo la kuipongeza kampuni ya matairi.
Pia usisahau, Bin Slum Tyres ilikuwa mdhamini wa timu zote mbili kongwe za Tanga, Coastal Union kupitia ufadhili wa mkurugenzi wake na baadaye African Sports.
Wakati wengi waliijua kupitia katika michezo, inaonekana Bin Slum Tyres imezidi kujitanua katika kurejesha katika jamii baada ya kuingia katika udhamini wa masuala ya usalama barabarani.
Bin Slum Tyres sasa imeamua kuwadhamini wanausalama kuhakikisha wanakuwa katika sehemu nzuri ambazo wanapokuwa wanapambana kwa ajili ya usalama wa Watanzania, basi angalau wanapata sehemu nzuri ya kupumzikia.
Kampuni hiyo imejenga takribani vibanda 30 katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia Dar es Salaam hadi mikoa mingine na askari wa usalama barabarani maarufu kama Trafiki nao wanakuwa wanapumzika.
Kila mmoja wetu anakubali kwamba trafiki wanajitahidi kufanya kazi yao kufanya mambo yaende.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bin Slum Tyres, Nassor Bin Slum, alikuwa mgumu kulizungumzia suala hilo akiamini si kila unaposaidia lazima uelezee, lakini baada ya kushawishiwa na gazeti hili kwa nia njema, alifunguka angalau kidogo.
“Kweli Bin Slum Tyres imeamua kutengeneza hivyo vibanda katika ubora sahihi na wa juu. Lengo ni kuungana na askari wetu wanapokuwa wakifanya jambo jema kwa ajili yetu.
“Unaona serikali ya awamu ya tano ilivyo imara, inavyowapigania wananchi. Sasa tukaona ni vizuri kuungana nayo pia kuipunguzia gharama katika maeneo tunayoona ni sahihi.
“Serikali inapambana kwa ajili ya wananchi, hivyo hakuna ubaya kwa wananchi kupambana kwa ajili ya serikali,” anasema.
Bin Slum anasema wametengeneza kila kibanda kwa zaidi ya Sh milioni 3, lakini wanachojivunia kwa si fedha.
“Fedha sawa, lakini tunachoangalia tumeshirikiana vipi na serikali kurudisha kwa jamii na hii ndiyo maana ya kufanya biashara hapa. Uliona tulianza katika michezo na bado tuko hapa lakini sasa tumekwenda katika jamii zaidi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment