December 28, 2017




Beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji ameiandikia barua klabu yake akitaka imuachie aende zake kutafuta maisha.

Haji ameindika barua akitaka Yanga imuachie aende kujiunga na klabu ya AFC Leopards ya Kenya ambayo tayari kumsajili.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Haji amesema ameona hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga, hivyo angependa kwenda kujiendeleza zaidi.

"Kama sina nafasi, maana yake sina msaada na sihitajiki. Hivyo kwa makubaliano mazuri bila ya kugombana acha niende nikajiendeleze.

"Kazi yangu ni soka na ninataka kujiendeleza. Siwezi kuendelea nikiwa benchi, hivyo Yanga nimewaandikia waniachie niwahi kujiunga na AFC Leopards," alisema.

Beki huyo alionyesha kiwango cha juu na kuisaidia Zanzibar Heroes kufika fainali ya Kombe la Chalenji lililomalizika wiki moja na ushee iliyopita.


1 COMMENTS:

  1. NI KWELI....:
    Akufukuzae akwambii toka..ndio msemo unaoweza kuutumia. Nani anaamini kuwa Gadiel ni Bora kuliko Mwinyi???mi wa kwanza siamni hili. Kinachombeba Gadiel ni Mapafu ya Mbwa na si uwezo wa kimpira. Katika uwezo uwanjani ni Mwinyi Haji. Mwinyi anajua...kama we ni muumini kweli wa mpira sidhani kama utabisha hilo. Mwinyi anajua kupiga hata krosi za kukadilia...ila Gadiel hilo kwake halipo.

    Mwinyi ana uwezo mzuri wa kumiliki mpira...ila gadiel hilo hana. Mwinyi ni mzuri hata katika mashambulizi lakini si Gadiel. Gadiel ni mzuri wa kufanya makingi. Mwinyi si mzuri kwenye kusaidia kukaba...anashindwa kusaidia beki zake za kati. Lakini Je...ndio hata michuano ya Kombe la Shirikisho asipate namba????hilo ndio tatizo langu...yaani ndio tumeona hafai kabisa???hata Nsajigwa nae hamuamini Mwinyi???

    Basi ni hatari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic