December 14, 2017


Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic amesema ana matumaini makubwa atafanya vizuri katika kibarua chake kipya na kuwashangaza wengi.

Logarusic maarufu kama Loga ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Sudam.

Akizungumza na SALEHJEMBE, moja kwa moja kutoka Sudan, Loga amesema yeye ni mtu anayeiamini kazi yake kuliko watu ambao wanaweza kujiuliza kuhusiana naye.

“Sijaja hapa (Sudan) kuwa nataka kubahatisha, nimekuja kufanya kazi na kufanya vizuri,” alisema.

“Mwanzoni nimeona shirikisho na watu wake wanataka kufanya vizuri, ninaamini nitapata ushirikiano wa kutosha na kufanya vema kwa niaba ya watu wa Sudan.”




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic