December 29, 2017

Bench la ufundi timu ya Pemba Kombaini;  Kushoto Meneja Steven Kapufi. Katikati ni Kocha Mkuu Mzee Abdallah na msaidizi wake Ussi Ally Juma.



Bench la ufundi timu ya Pemba Kombaini linaamini lazima kikosi cha Zanzibar Heroes, kitalala dhidi yao.

Kocha Mkuu wa Pemba Kombaini, Mzee Abdallah amesema vijana wake wako vizuri sana.

Timu hizo zinakutaka leo katika mechi ya kirafiki itakayopigwa kwenye Uwanja wa Gombani mjini Pemba.

Meneja wa Pemba Kombaini, Steven Kapuf naye ameisisitiza, wana imani kubwa ya kuifunga Zanzibar Heroes katika mechi hiyo ya leo.

Zanzibar Heroes walifanikiwa kufika hadi fainali ya michuano ya Chelenji iliyofanyika nchini Kenya, wiki mbili zilizopita.


1 COMMENTS:

  1. UNAPATA PICHA GANI KWENYE HILI.....:::
    Pemba wanapeleka Pemba Kombaini uwanjani ili kushindana na Zanzibar Heroes. Inawezekana mimi peke yangu sijaelewa...ila kwa mtu aliyeelewa nahisi hawezi pata shida..na kwa mtu ambae hajaelewa kama mimi lazima apate shida. Kwanini Pemba Kombaini????kuna nini hapo???je Jamii ya Pemba imeona kuna kitu hapo???na ni kitu gani???

    Nimehisi nao Pemba wanataka kuonesha kwamba hata kwao pia wachezaji wapo na si Unguja tu. Ndio maana wamekuja na wazo lao la kuleta timu yao...maana unaweza ukahisi ni timu ya Taifa yao. Katika michezo kuna figisu nyingi sana. Na ili kila mtu alidhike anahitaji kufanya kile anachohisi ni bora kwa wakati huo.

    Pemba Kombaini....???!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic