Sasa ni uhakika kwamba Zanzibar Heroes watarejea kwa ndege au "mwewe" wakitokea Kenya hadi Zanzibar.
Kabla wakati timu hiyo ikisafiri kwenda nchini Kenya kwa ajili ya michuano ya Chalenji, walipanda basi wakitokea Dar es Salaam.
Lakini kutokana na mwenendo wao mzuri katika michuano ya Chalenji wakiwa wamecheza na kushinda mechi mbili, sare moja na kupoteza moja katika hatua ya makundi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema lazima watarejea kwa usafiri wa ndege.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rashid Ali Juma amesema kikosi hicho kitwae kombe au la, kitapanda ndege.
“Kwa hapa tulipofikia, hatutajali wamechukua kombe au hapa. Hatutaangalia wamefanya nini baada ya hapa, kikubwa wakati wanarejea lazima wapande ndege kuonyesha tumeuthamini mchango na heshima wanaotoa kwa taifa letu,” alisema.
NIWAAMBIE SIKU INGINE ILI MSIRUDIE TENA:-
ReplyDeleteIli timu ifanye vizuri inahitaji maandalizi ya dhati na kuthaminiwa na ngazi zote katika jamii. Mimi sipendi mtoto hadi kafanya vizuri darasani ndio nimpongeze ila namuandalia mazingira mazuri ya kufanya vizuri kwanza. Niulize..."kwahiyo wajomba zangu wangefanya vibaya je mngewaaambiaje au ndio mngesema kila mtu atafute nauli yake mwenyewe?".
Siku ingine muanze kuiandaa timu mapema na si hadi wafanye vizuri. Ipeni motisha ili hata ikifanya vizuri mnaweza kujisifia.