December 12, 2017


Kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim amefiwa na mtoto wake.

Mo Ibrahim amepata pigo baada ya mwanaye kufariki dunia katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza mtoto huyo alikuwa mgonjwa lakini juhudi za kuokoa maisha yake hazikuzaa matunda.


Msemaji wa Simba, Haji Manara ametoa salamu za pole kwa Mo Ibrahim kwa niaba ya klabu hiyo.

BLOG YA SALEHJEMBE INATOA POLE KWA MO KUTOKANA NA MSIBA ULIOMPATA.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV