December 31, 2017



Mshabiki mbalimbali wa Simba wameanzisha mjadala mitandaoni namna ambavyo kikosi chao kilivyofunga mwaka kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC.

Kikosi hicho kilionyesha safi mwanzoni mwa kipindi cha kwanza, lakini baada ya dakika 15 kikapotea na kutoa nafasi kwa Ndanda FC kutawala karibu kipindi chote.

Hata hivyo, katika kipindi cha pili, Simba ilikianza kwa kasi na kufanikiwa kuizamisha Ndanda kwa mabao mawili, yote yakifungwa na nahodha wake, John Raphael Bocco.

Pamoja na ushindi huo, gumzo ulikuwa ule mfumo wa 3-5-2 ambao Simba walioutumia chini ya Kocha Irambona Masoud Djuma ambaye ndiye ameanza kuifundisha Simba kama kocha mkuu baada ya Joseph Omog kutupiwa virago.

Mijadala mingi pia ilihusisha mfumo huo kama ni sahihi, kwa kuwa wengi waliingia hofu katika kipindi cha kwanza lakini baadaye walionekana kama kuelewa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic