December 27, 2017




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kila mashindano yakiwemo ya mchangani yatalazimika kuombewa vibali ili kufanyika.

Rais wa TFF, Wallace Karia amesema mashindano hayo huwa hayaibui vipaji kwa utaratibu.

Hivyo amesisitiza, hata wale wabunge au wanasiasa wamekuwa wakiandaa mashindano mbalimbali, watalazimika kuomba vibali.

"Hatutakata kabisa, tuna kanuni tunatengeneza ili kuhakikisha kila mashindano yanayoandaliwa, basi yawe na faida kwa vijana.

"Angalia unandaa mashindano ya wachezaji wastaafu ambao wametoka katika Premier League, faida yake nini," alisema Karia.

Hata hivyo, suala hilo tayari linaonekana kupokelewa tofauti na wadau wa soka nchini ambao wengi wanaona jambo hilo si sahihi kwa kuwa soka inatakiwa kuwa huru na hasa katika mashindano mengi ya mchangani ambayo hayakuwa yakiharibu lolote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic