Kocha mkuu Yanga, George Lwandamina na mshambuliaji Obrey Chirwa tayari wako Zanzibar.
Lwandamina na Chirwa wameungana na kikosi hicho wakati timu itakuwa ikikipiga katika mechi ya nusu fainali dhidi ya URA ya Uganda.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa, jana Jumanne Chirwa alikutana na viongozi wa Yanga akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika na kuzungumzia namna ya kulimaliza suala lake la malipo ya fedha za usajili.
Baada ya kikao hicho, Chirwa akawa anasubiri kusafirishwa kwenda Zanzibar na leo ameungana na kikosi.
Awali jana, kuhusiana na kuungana na wenzake huko Zanzibar, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alisema: “Kama kocha atamuhitaji basi ataungana na wenzake, kama unavyojua hajafanya mazoezi na wenzake kwa muda mrefu, hivyo tunasubiri uhitaji wa kocha, akisema anamuhitaji atakwenda.”
0 COMMENTS:
Post a Comment