January 31, 2018




Kocha Mkuu wa Singida United, Hans Pluijm wikiendi iliyopita alijikuta katika hali tete baada ya shabiki kumchukulia begi lake wakati wakiwa wanashangilia ushindi.
Singida ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons ambalo lilikuwa la dakika za mwisho hali iliyosababisha  kocha huyo kushangilia kwa nguvu ka kuondoka kwenye benchi.

Singida ambayo ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 27 imepanda daraja msimu huu kwa kasi ikiwa inawania kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Mtendaji Mkuu wa Singida United, Festo Sanga amesema kuwa, tukio hilo lilitokea uwanjani wakati timu hiyo iliposhinda bao la jioni hali iliyosababisha mashabiki kumyanyua kocha juu juu ndipo shabiki mmoja alipoamua kulichukua begi hilo.

“Awali kocha alijua ameibiwa begi, kwani bao tulilokuwa tumelifunga lilikuwa la jioni na hatukutarajia kupata ushindi, ndipo mashabiki walipomyanyua kocha Hans juujuu huku wakishangilia naye ndipo shabiki mmoja akachukua begi hilo na kukaa nalo pembeni.


 “Hadi mpira unamalizika kocha hakuweza kuliona begi lake akadhani ameibiwa aliondoka hadi kambini, lakini baadaye shabiki huyo alilileta likiwa salama,” alisema Sanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic