January 17, 2018


MPIRA UMEKWISHAAA

-KADI Yondani analambwa kadi ya njano baada ya kucheza kindava-Ajibu upande wa Yanga, Uwesu na kipa Massawe upande wa Mwadui pia wako chini wakitibiwa


DAKIKA 3 ZA NYOMGEZA 
Dk 90, Kipa Masawe anaruka vizuri kudaka krosi ya Mwinyi
Dk 89 Nonga anaachia mkwaju mkali hapa, unapiga nyavu za nje
Dk 88, Kessy anaachia mkwaju mkali kabisa lakini unapita juuuuu, goal kick
Dk 85 Buswita analambwa kadi ya njano kwa kucheza kindava
Dk 84 Nkomola anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini Mgevege anaokoa na kuwa kona. Inachongwa vizuri hapa, haina faida
Dk 83, Said Juma anaruka vizuri lakini anashindwa kuuwahi mpira ambao kama angeugusa, ingekuwa hadithi nyingine kwenye lango la Mwadui


SUB Dk 80 Mwadui FC wanafanya mabadiliko kwa kumtoa Morriss Malaki na nafasi yake inachukuliwa na Athuman Rajab
SUB Dk 77, Yanga wanamtoa Mahadhi na nafasi yake inachukuliwa na Yohana Nkomola
Dk 73 Mwadui wanapoteza nafasi nyingine nzuri kupitia Agustus ambaye anashindwa kujiamini akiwa karibu na lango la Yanga
Dk 71, Mwinyi naye anajaribu na mkwaju wake mkali unamshinda kipa lakini anauwahi na kudaka tena

Dk 69, Kessy anaachia mkwaju mkali kabisa lakini unatoka nje sentimeta chache kabisa


SUB Dk 68, Yanga wanamuingiza Raphael Daud na wanamtoa Said Juma Makapu
Dk 65, Ajibu anachonga kona na Mwadui wanaokoa vizuri hapa
Dk 65, Ajibu anachonga vizuri, Yondani anaachia mkwaju hapa inakuwa kona tena
Dk 63, Mgeveke anamdhibiti vizuri Mahadhi, mpira unakuwa kona na wote wako chini pale
Dk 58, Luhende anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mzuri wa Mahadhi ulimfikia Buswita na kuwa kona ya nne


Yanga hii leo. Inachongwa na Ajibu na kipa Mwadui anadaka kwa ustadi mkubwa
Dk 57 Buswita anaachia mkwaju mkali kabisa lakini anapiga juuuuuu
Dk 56 Mahadhi anaingia vizuri kabisa lakini Mwadui FC wanakuwa makini kuokoa
SUB Dk 55 Mwadui wanafanya mabadiliko, Jean Marie anakwenda benchi upande wa Mwadui anaindia Moses Malaki
Dk 52, Nonga anaruka juu na kupiga kichwa mpira wa krosi lakini unakwenda nje na kuwa goal kick
Dk 50, Ajibu anaingiza mpira safi kabisa wa faulo, lakini wanashindwa kuwahi na kipa Mwadui FC anadaka


SUB Dk 49 Amissi Tambwe aliyeumia baada ya kuwekwa chini, anaingia Said Juma 'Ronaldo'
Dk 48 Tambwe anawekwa chini baada ya kumtoka mlinzi mmoja wa Mwadui, faulo
DK 47, Nonga anagongana na mwenzake wakati wakijaribu kumalizia
Dk 45 mpira umeanza na Mwadui FC wanaanza kwa kugongeana vizuri lakini Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Mwadui FC.


MAPUMZIKO
-Nonga anamtoka vizuri kabisa Vicent lakini shuti lake linapaa juuu

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Yanga wanapata faulo karibu kabisa na lango la Mwadui, inachongwa, Mwadui wanaokoa
Dk 43 sasa, hakuna mashambulizi makali ya kutisha, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja
Dk 41 Said Juma Makapu analambwa kadi ya njano kwa kucheza kindava
Dk 37, Ajibu anaachia mkwaju mkali wa adhabu, kipa anapangua unagonga mwamba hapa, ilikuwa hatari kabisa
Dk 33, Tambwe anapoteza nafasi nzuri tena baada ya kupokea krosi nzuri kabisa
Dk 28 Awessu anaoenakan kutawala zaidi katikati akiwasumbua viungo wa Yanga


Dk 23, Tambwe anapoteza nafasi nzuri baada ya kushindwa kuuwahi mpira
Dk 18, Yanga wanaonekana wanaanza kubadilika taratibu na kucheza vizuri
Dk 14, Yanga wanapata kona nyingine baada ya Awadhi Juma kulazimika kutoa, inachongwa lakini haina faida


Dk 10, Mwadui wanajisalimisha kwa kutoa mpira nje inakuwa ni kona, inachongwa na Ajibu 
Dk 7, Mwadui wanafanya shambulizi jingine lakini bado krosi zao hazifiki katikati
Dk 4 Mwadui FC wanapata mkwaju wa adhabu lakini unapigwa kizembeee na Seseme
Dk 3, kama Tambwe angekuwa makini, basi ilikuwa ni hatari sana kwa Yanga

Dk 1, Yanga ndiyo wanaonekana kushambulia kwa kasi zaidi ingawa MWadui wako makini

1 COMMENTS:

  1. Benchi zima la ufundi Yanga liondolewe haraka sana kama kweli tunataka kutetea ubingwa, maporo wote wapigwe chini isipokuwa Tshitshimbi, yaani kuanzia Rostam,Ngoma,Tambwe, Kamusoko na Chirwa wote out

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic