January 17, 2018




Kocha George Lwandamina amelazimika kukaa jukwaani wakati timu yake ikipambana na Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Lwandamina alikuwa jukwaani na mmoja wa viongozi wa Yanga Omary Kaaya wakati Yanga ikipambana na Mwadui na taarifa zinasema kibali chake cha kazi kimeisha.

"Juhudi zinaendelea na kibali kitapatikana hivi karibuni kwa kuwa uongozi ulishaanza kushughulikia," kilieleza chanzo.

Kocha huyo raia wa Zambia, hivi karibuni alikuwa katika wakati mgumu alipolazimika kurejea kwao baada ya kufiwa na mwanaye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic