January 22, 2018



FULL TIME
Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba wanaibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Dk ya 90+4: Kipa wa Kagera anauwahi mpira an kuudaka, kidogo Okwi aipatie Simba bao.
Dk ya 90+4: Muda wowote mchezo utamalizika.
Dk ya 90: Sasa ni muda wa dakika za nyongeza.
Dk ya 89: Kagera wanafika langoni mwa Simba lakini inakuwa offside.
Dk ya 87: Simba wanapambana kutafuta bao la tatu.
Dk ya 86: Simba wanajiandaa kumuingiza Laudit Mavugo. 
Dk ya 82: Mchezo umechangamka.
Pasi nzuri ya Kapombe inatua kwenye mwili wa John Bocco ambaye anatupia wavuni. Simba mbili.
Dk ya 79: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 78: Kichuya anamiliki mpira eneo la katikati ya uwanja.
Dk ya 75: Kasi ya mchezo imeongezeka.
Dk ya 71: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Gyan anaiongia Shomari Kapomb.
Said Ndemla anaipatia Simba bao kwa shuti ambalo linajaa wavuni moja kwa moja.
Dk ya 69: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 63: Nguvu ya Kagera inaongezeka.
Dk ya 60: Pastory Athanas anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Christopher Edward, upande wa Kagera.
Dk ya 53: Juuko Murshid wa Simba anapata kadi ya njano kwa kucheza vibaya.
Dk ya 50: Simba wanaanza kuongeza kasi.
Dk ya 48: Mchezo umeanza kwa timu zote kusomana.
Kipindi cha pili kimeanza.

 MAPUMZIKO

Dk ya 45 + 2: Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza.
Dk ya 45 + 1: Kagera wanapata kona, inapigwa lakini haina faida.
Dk ya 45: Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.
Dk ya 44: Kasi ya mchezo imepungua.
Dk ya 40: John Bocco wa Simba anapata kadi ya njano.
Dk ya 39: Simba wanashambulia, Okwi anahusika lakini kipa Juma Kaseja anafanya kazi nzuri.
Dk ya 38: Kagera wanashambulia lwango la Simba.
Dk ya 35: Okwi anapiga faulo inatoka nje.
Dk ya 34: Kadi ya njano kwa Mohamed Fakh wa Kagera Sugar.
Dk ya 31: Asante Kwasi anatoa mpira inakuwa kona kwa Kagera.
Dk ya 26: Ndemla anapiga pasi lakini inanaswa.
Dk ya 25: Simba wanafanya shambulizi kali lakini Kagera wanakuwa makini.
Dk ya 20: Kagera wanaanza kushambulia kwa kasi lakini Simba wapo makini.
Dk ya 18: Faulo inapingwa nje ya boksi la Kagera Sugar, mpira unaokolewa.
Dk ya 15: Simba wanapata kona.
Dk ya 10: Hakuna mashambulizi makali. 
Dk ya 8: Juma Nyosso wa Kagera Sugar anapewa kadi ya njano kwa kumzonga mwamuzi.
Dk ya 6: Wachezaji wa Kagera wanamzonga mwamuzi. 
Dk ya 4: Timu zote zimeanza kwa kasi ya kawaida.

Dk ya kwanza: mchezo umeanza.

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic