January 24, 2018



Kocha wa zamani wa Simba na sasa timu ya Taifa ya Sudan, Mcrotia Zdravko Logarusic (Loga) amefanikiwa kuipeleka timu yake hatua ya robo fainali ya michuano ya Chan inayofanyika nchini Morocco.

 Sudan imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kutoka sare na wenyeji wa michuano hiyo Morocco,  katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi .

 Akizungumza Kutoka Morocco, kocha huyo alisema  haikuwa kazi rahisi na atapambana kuhakikisha anafanya vyema na kusonga mbele japo si kazi rahisi.


“ Nashukuru vijana wangu wamepambana na kuvuka hatua ya makundi lakini pia tumefika hatua ya robo fainali na lengo letu na kufika hatua ya mwisho ya michuano hii japo ni migumu,” alisema Loga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic