January 11, 2018


Unaweza kusema ni habari njema kwa kuwa afya ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta aimeimarika kwa kiasi kikubwa na sasa anaweza kupambana uwanjani.

Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji alikuwa nje kwa takribani miezi miwili akiuguza goti lake lakini sasa amerejea uwanjani na anacheza soka la ushindani.

Kabla ya kurejea uwanjani, Samatta alianza kujifua kwenye gym ya klabu hiyo, baadaye akatumia vifaa mbalimbali akiwa katika usimamizi wa daktari.

Baada ya hapo alirejea uwanjani lakini alikuwa akifanya mazoezi mepesi kabla ya sasa kuingia uwanjani na kupambana kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic