Mashabiki mbalimbali wa klabu ya Difaa Al Jadid wameonyesha kufurahishwa na Saimon Msuva kusaidia watoto yatima.
Lakini kingine kilichowafurahisha zaidi ni kuona Msuva akikabidhi jezi ya timu yao kwa mlezi wa watoto hao yatima katika kituo cha Sinza jijini Dar es Salaam.
Kupitia mitandao ya kijamii ya mashabiki wa klabu hiyo, wamemsifia Msuva kwa moyo wa ukarimu kwa watoto wenye shida.
Wengi wameshea picha hiyo na kusema moyo huo ndiyo moyo wa watu wote walio ndani na karibu ya Difaa Al Jadid.
Baada ya kupata mapumziko kutoka Morocco, Msuva alirejea nchini kwa mapumziko na siku chache baadaye aliamua kuwatembelea watoto na kuwapa misaada.
Msuva amekuwa kati ya wachezaji wanaofanya vizuri na kikosi hicho tokea amejiunga nacho akitokea Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment