January 17, 2018



Timu ya Polisi Tanzania inaondoka kesho Ijumaa tarehe 29/12/2017 Jijini DSM kuelekea Mkoani Mbeya kuwakabili Mbeya Kwanza katika mechi ligi daraja la kwanza kundi B itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 31/12/2017.

Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisa Habari na Mawasiliano wa Polisi Tanzania , Frank Geofray amesema msafara huo utakuwa na wachezaji 20 na Viongozi  7 utaondoka alfajiri ili kuwahi Mbeya kuizoea hali ya mkoa huo.

Amesema wamefanya maandalizi ya kutosha ikiwemo kukamilisha taratibu zote za wachezaji waliowasajili katika dirisha dogo la usajili.

"Hali ya kikosi ni nzuri na kina morali ya hali ya kutoka na ushindi dhidi ya Mbeya Kwanza hivyo tutarajie ushindani wa hali ya juu katika mchezo huo" Alisema Geofray.

Kwa Upande wake Kocha wa timu hiyo Ali Bushiri amesema anaingia Mbeya kwa lengo la kusaka point 3 tu na hakuna lingine ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia Ligi kuu mwakani.

Amesema timu yake imefanya mazoezi ya kutosha hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanayafanyia kazi yale yote aliyowafundisha ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.


Timu ya Polisi TZ ipo katika nafasi ya pili huku ikiwa imejikusanyia alama 16 katika michezo 9 iliyokwisha kucheza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic