January 22, 2018


Shabiki anayedaiwa kushambuliwa na beki wa Kagera, Juma Said Nyosso ililazimika apewe huduma ya kwanza chini alipokuwa amelala katika uwanja wa Kaitaba mjini Kagera.

Shabiki huyo inadaiwa alishambuliwa na Nyosso mara tu baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Kagera Sugar dhidi ya Simba kwisha.



Watoa huduma ya kwanza, walichukua takribani dakika nane kumpatia huduma shabiki huyo aliyezimia.


Nyosso anashikiliwa na Polisi mkoani Kagera baada ya kudaiwa kumshambulia shabiki huyo kwa ngumu hadi kuzirai.

1 COMMENTS:

  1. Hii itakuwa ni fundisho kwa mashabiki wengine wasio jua joto la mpira lilivyo. Watu wengine si wastaarabu ndio maana hadi leo bado tuna mfumo wa kutengana majukwaa hapa Tanzania. Washabiki wengi hawajui maana ya ushabiki kabisa. Hili ndilo wanalotaka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic