January 10, 2018




Pamoja na Simba kupoteza mechi ya pili mfululizo na kuondolewa katika michuano ya Mapinduzi, mashabiki wa Simba hilo halikuwazuia kumvaa beki wao mpya, Asante Kwasi na kupiga naye picha “pwaaaa”.

Mashabiki hao walionekana ni wenye furaha mara baada ya Simba kuwasili bandarini jijini Dar es Salaam ikitokea Zanzibar, jana.

Hata kabla ya kuingia kwenye basi, mashabiki hao walimvaa Kwasi na kupiga naye picha kwa mtindo wa “Selfie” hadi alipopanda basi.


Lakini baadaye, Kwasi aliteremka kwenye basi akiwa na wenzake na kuanza kutembea na mashabiki hao wakamfuata tena na kumvaa wakitaka “selfie”.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic