January 19, 2018

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Maadili imetoa adhabu kali kwa baadhi ya viongozi wanaosimamia mpira wa mkoani Mtwara kutokana na ubadhilifu wa fedha za mapato zilizopatika katika kipute cha Ndanda dhidi ya Simba.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Hamid Mbwezeleni amesema kuwa kwenye mechi hiyo, fedha zilizopatikana haziendani, kwani mara ya kwanza karatasi zilizofika katika shirikisho hilo zilikuwa zinaonyesha kiasi cha shilingi milioni 37 ndiyo zilipatikana na karatasi nyingine inaonyesha kiasi cha shilingi milioni 34 ndiyo zilipatikana.


“Kamati ya Maadili tulikaa juzi na kujadiliana juu ya mechi iliochezwa mkoani Mtwara kati ya Simba na Ndanda ambapo kuna tuhuma zinaonyesha kuna ubadhilifu wa pesa zilizopatikana katika mechi hiyo kwani karatasi ya kwanza inaonyesha pesa zilizopatikana ni kiasi cha shilingi milioni 37 na kandarasi ya pili inaonyesha kuwa ni kiasi cha milioni 34, sasa tunataka kujua mwisho wake ilikuwaje na kuna watu mbalimbali walihusishwa huenda wao ndiyo wamechukua.

“Hivyo, kamati ya maadili tumekaa na kujadiliana na watu waliousishwa ni watu wa nne ambao ni Selemani Kachele ambaye ni Katibu wa Ndanda na moja kati ya viongozi wa mpira Mtwara kwani yeye aliitwa kwenye kikao huko cha kuhesabu pesa kwani kuna bi mkubwa mmoja alikuwa anadai pesa kuwa hajalipwa lakini Katibu wa mkoa huo aligomea kutoa hizo pesa na kudai kuwa hawadaiwi.

“Lakini kwenye mgao watu wa mkoa huo walikaa na yule mwanamke na bado hatujajua kama alilipwa au la lakini Selemani Kachele haijulikani kama na yeye ameusishwa kwani haionyeshi kama ile pesa imelipwa au la kwa hiyo huyu sisi hatujamuadhibu hivyo tunamuacha.

“Wa pili kati ya hao watuhumiwa ni Selemani Kahumbi yeye ni mweka pesa wa timu ya Simba na huyu bwana naye alikwenda kule kama mwakilishi wa Simba kuangalia mapato yao waliopata lakini naye wamehisi labda naye amechukua.

“Wa tatu ni Kizito Mbano, huyu ni katibu wa TFF wa Mtwara na alikuwa anazifahamu tofauti hizo zilizotokea za pesa na walishirikiana na mkuu wa kituo cha huko Dastani Mkumbi na wao ndiyo waliotoa taarifa hizi mara mbili na tulipowahoji ndiyo wakatoa information za pesa kuchukuliwa,” alisema.

Aidha, aliongeza kuwa viongozi hao moja wao ambaye ni Kizito Mbano yeye wameamua kumfungia miaka mitano ya kutojihusisha na mchezo wa soka kwani yeye aliamua kuwa kimya licha ya kujua kila kitu na mtu wa mwisho ni Dastani Mkumbi yeye kwa ushahidi waliopata kutoka kwa mashahidi ndiyo aliopokea pesa na kabla ya kuzipeleka Dar es Salaam aliamua kubadilisha karatasi hivyo yeye wameamua kumfungia maisha kutojihusisha na mchezo wa soka tena.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic