January 27, 2018



Real Madrid imeanza kukubali kwamba kikosi chake ni dhoofu el hali.

Hivyo intake kujiboresha baada ya kuamua kutenga pauni million 500 kuanza usajili wa kuaminika.

Katika ya wachezaji ambao inawataka, wa kwanza ni Eden Hazard wa Chelsea ambaye imemtengea pauni million 200.

Mshambuliaji Harry Kane, Mwinginereza anayekipiga Tottenham, yeye ametengewa pauni million 200 pia. Huku kipa namba moja wa Manchester United, David de Gea ambaye ametakiwa kwa muda sasa na Madrid, katengewa pauni million 100.

Mabingwa hao wa dunia, mabingwa wa Ulaya pia wamekuwa wakienda mwendo wa kusuasua katika La Liga na unaonekana ni msimu mbaya zaidi chini ya Kocha Zinedine Zidane.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic