Klabu ya Yanga imeishauri kamati ya maandalizi ya Kombe la Mapinduzi kutengeneza utaratibu mzuri ambao hautakuwa ukiwaumiza wachezaji wa timu zinazoshiriki michuano hiyo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kucheza mechi mfululizo katika michuano hiyo si jambo zuri kwa wachezaji kiafya.
“Wanaweza kuweka utaratibu mzuri katika michuano ijayo ili kuwaepusha wachezaji kucheza mechi nyingi sana mfululizo katika kipindi kifupi,” alisema Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha.
“Wakae waliangalie hili kwa faida ya wachezaji ambao pia wanakuwa wana majukumu baada ya michuano hii.”
Yanga ilitolewa hatua ya nusu fainali katika Kombe la Mapinduzi baada na URA ya Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment