January 12, 2018



Kikosi cha Ndanda FC kipo tayari kuwavaa wageni wao Mbao FC na kubeba pointi zote tatu.

Ndanda FC watakuwa wenyeji wa timu ngumu ya Mbao FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, kesho.

Msemaji wa Ndanda FC, Idrisa Bandari amesema wanaujua ubora wa Mbao FC lakini wao wana kikosi bora zaidi na wanachotaka ni pointi tatu.

"Mbao FC ni timu nzuri, tunaliheshimu hilo. Lakini sisi tuna kikosi bora na kwa kuwa tuko nyumbani tutakachotaka ni kutumia nafasi hiyo kushinda pointi tatu," alisema.

Tayari Mbao FC wako mjini Mtwara kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao kila timu itataka kushinda.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, wenyeji Ndanda FC wako katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 11 na wageni wao Mbao FC wana pointi 14 katika nafasi ya 14 .


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic