Azam FC imeweka mambo hadharani na kusema iko tayari kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya Simba.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kikosi chao kipo tayari baada ya maandalizi ya kutosha chini ya kocha wake raia wa Romania, Artisca Cioba.
"Maandalizi yameenda vizuri na sasa tunachosubiri ni mechi yenyewe," alisema.
"Hadi sasa tumepoteza mechi moja lakini tuna imani tumerejea katika kasi yetu baada ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi kuu kwa ushindi wa mabao matatu bila."
Azam FC ina kibarua dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Simba ambao wanakutana na Azam FC kwa mara ya pili msimu huu baada ya sare kwenye mechi ya kwanza.
Azam wapo tayari ila Marefa wa mchezo wa kesho lazima wamuangalie vizuri Agrey Moris na mchezo wake wakutaka kuuwa wenzake. Mchezo ni furaha sio vita wala kick boxing.
ReplyDelete